Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Elly Marko Macha

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. ELLY M. MACHA aliuliza:- Katika miaka ya 60 na 90, Serikali yetu kwa ufadhili wa nchi rafiki kama Norway na Sweden ilijenga vyuo vya ufundi vilivyotoa mafunzo mbalimbali kwa watu wenye ulemavu hapa nchini kama vile Yombo - Dar es Salaam, Singida, Mtapika – Masasi, Masiwani – Tanga, Mbeya, Ruanzari – Tabora na Mwirongo-Mwanza; hivi sasa kati ya vyuo saba ni vyuo viwili tu vya Yombo na Singida ndiyo vinafanya kazi tena kwa kusuasua:- (a) Je, ni sababu zipi zilizosababisha vyuo hivyo vitano vifungwe wakati kuna mahitaji makubwa ya watu wenye ulemavu kupata mafunzo ya ufundi? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kufungua haraka vyuo hivyo vilivyofungwa ili viendelee kutoa mafunzo ya ufundi kwa watu wenye ulemavu? (c) Ili kutoa fursa zaidi za mafunzo ya ufundi kwa watu wenye ulemavu, je, Serikali ina mkakati gani wa kujumuisha watu wenye ulemavu kwenye vyuo vyake vya VETA na FDC?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. ELLY M. MACHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Napenda kusema tu kwamba sikuridhika kabisa na nina hakika watu wenye ulemavu hawakuridhika kabisa na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri ambayo ameyatoa. Ina maana kwamba kwa kutokuwa na miundombinu au kutokuwa na watumishi ni sababu ya kutosha ya kusababisha vyuo vifungwe kwa miaka mingi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la kwanza. Naomba Mheshimiwa Naibu Waziri atupe concrete sababu kwa nini vyuo vimefungwa na vitafunguliwa lini, atupatie time frame.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, hawa watumishi ambao anasema wanatayarishwa, tunahitaji muda gani kuwatayarisha hawa watumishi kwa sababu watu wenye ulemavu wamekuwepo na vyuo vimekuwepo miaka mingi lakini vimefungwa kwa miaka mingi na inaonekana kama ni business as usual but it is not business as usual. Ahsante.

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kimsingi, pamoja na kufungwa kwa vyuo hivyo jambo ambalo tayari limeshatolewa ufafanuzi namna gani litafanyika, kupitia mfumo wa elimu jumuishi sasa hivi vyuo vyote vya ufundi ikiwemo VETA, FDC lakini hata shule zinazotoa mafunzo ya ufundi tunahakikisha kwamba tunazingatia namna tunavyoweka miundombinu na namna ya kufundisha kwamba watu wenye ulemavu wanazingatiwa. Hao nawazungumzia hasa wale vijana wenye umri wa kuweza kuingia katika vyuo hivyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo niseme tu kwamba, kwa hali ya sasa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia lakini pia kupitia ngazi zetu za juu kama tulivyoona Ofisi ya Waziri Mkuu, tunahakikisha kwamba walemavu wanapewa kipaumbele cha hali ya juu na yeye atakuwa shahidi hata sasa tunapotoa kwa mfano karatasi zetu humu Bungeni au taarifa zozote lazima tuzi-print kwa nukta nundu na mambo mengine. Kwa hiyo, walemavu wanapewa fursa nyingi na tunawajali kupita kiasi katika kila ngazi. Naomba atuvumilie aone namna ambavyo tutaweza kuendelea katika kuhakikisha tunarekebisha hali ambazo zipo.

Name

Amina Saleh Athuman Mollel

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. ELLY M. MACHA aliuliza:- Katika miaka ya 60 na 90, Serikali yetu kwa ufadhili wa nchi rafiki kama Norway na Sweden ilijenga vyuo vya ufundi vilivyotoa mafunzo mbalimbali kwa watu wenye ulemavu hapa nchini kama vile Yombo - Dar es Salaam, Singida, Mtapika – Masasi, Masiwani – Tanga, Mbeya, Ruanzari – Tabora na Mwirongo-Mwanza; hivi sasa kati ya vyuo saba ni vyuo viwili tu vya Yombo na Singida ndiyo vinafanya kazi tena kwa kusuasua:- (a) Je, ni sababu zipi zilizosababisha vyuo hivyo vitano vifungwe wakati kuna mahitaji makubwa ya watu wenye ulemavu kupata mafunzo ya ufundi? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kufungua haraka vyuo hivyo vilivyofungwa ili viendelee kutoa mafunzo ya ufundi kwa watu wenye ulemavu? (c) Ili kutoa fursa zaidi za mafunzo ya ufundi kwa watu wenye ulemavu, je, Serikali ina mkakati gani wa kujumuisha watu wenye ulemavu kwenye vyuo vyake vya VETA na FDC?

Supplementary Question 2

MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi nami niweze kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa changamoto katika suala zima la elimu na hasa elimu jumuishi kwa watu wenye ulemavu ni kutokana na uhaba wa walimu katika vyuo mbalimbali hasa vyuo vikuu hapa nchini. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha kwamba katika vyuo vyote vikuu hapa nchini vinakuwa na programu mahsusi kabisa kwa ajili ya kuwafundisha walimu watakaokwenda kuwafundisha wanafunzi wenye ulemavu hapa nchini ili tuondokane na tatizo hili la uhaba wa walimu pamoja na kuhakikisha kwamba ajira zinakuwepo kwa watu wenye ulemavu? Ahsante.

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza ili kufanikisha hilo, kwa mfano ukiangalia katika utoaji wa mikopo safari hii watu wenye ulemavu wote kwa ujumla wake bila kujali fani anayochukua wamepewa mikopo. Pili, tunacho chuo maalum, Chuo cha Patandi - Arusha ambacho ni kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa walimu ambao wanaenda kuwafundisha wanafunzi wenye ulemavu. Hali kadhalika, kwa upande wa vyuo vikuu tunayo maeneo ambayo yanahusika katika kuzingatia ufundishaji wa walimu kwa ajili ya watu wenye ulemavu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ujumla wake niseme tu kwamba eneo hili ni pana sana kwa sababu linahitaji walimu wa aina tofauti tofauti kwa ajili ya kufundisha watu wenye ulemavu wa aina tofauti tofauti. Kwa hiyo, ukiwachukua kwa ujumla wake useme kwamba walimu wenye ulemavu labda 200 ukafikiria ni wengi, hawatakuwa wengi kwa sababu mahitaji ya wale wanaoenda kuwafundisha inakuwa wanafunzi ni wachache katika eneo fulani lakini yale maeneo ni mengi sana. Kwa hiyo, juzi tu mimi mwenyewe nimefuatilia pale Patandi na kuona ni jinsi gani tutaweza kurekebisha hasa miundombinu na kuwawezesha walimu wengi zaidi. Ahsante.

Name

Stella Ikupa Alex

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. ELLY M. MACHA aliuliza:- Katika miaka ya 60 na 90, Serikali yetu kwa ufadhili wa nchi rafiki kama Norway na Sweden ilijenga vyuo vya ufundi vilivyotoa mafunzo mbalimbali kwa watu wenye ulemavu hapa nchini kama vile Yombo - Dar es Salaam, Singida, Mtapika – Masasi, Masiwani – Tanga, Mbeya, Ruanzari – Tabora na Mwirongo-Mwanza; hivi sasa kati ya vyuo saba ni vyuo viwili tu vya Yombo na Singida ndiyo vinafanya kazi tena kwa kusuasua:- (a) Je, ni sababu zipi zilizosababisha vyuo hivyo vitano vifungwe wakati kuna mahitaji makubwa ya watu wenye ulemavu kupata mafunzo ya ufundi? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kufungua haraka vyuo hivyo vilivyofungwa ili viendelee kutoa mafunzo ya ufundi kwa watu wenye ulemavu? (c) Ili kutoa fursa zaidi za mafunzo ya ufundi kwa watu wenye ulemavu, je, Serikali ina mkakati gani wa kujumuisha watu wenye ulemavu kwenye vyuo vyake vya VETA na FDC?

Supplementary Question 3

MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu ya Mawaziri, kuna hivi vyuo viwili Chuo cha Yombo na Chuo cha Singida, pamoja na uwepo wa vyuo hivi viwili lakini bado kuna changamoto nyingi sana ambazo zinavikabili vyuo hivi. Naomba niongelee specific Chuo cha Yombo kwa sababu ni chuo ambacho nimekitembelea. Chuo hiki kina changamoto ya deni kubwa la umeme, miundombinu chakavu pamoja na vifaa vya kujifunzia na kufundishia. Naomba nisikie kauli ya Serikali ni hatua gani za haraka na za makusudi za kunusuru vyuo hivi ili visije vikafungwa kama ambavyo vimefungwa hivi vyuo vingine? Ahsante.

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwa upande wa chuo hicho nikiri pia hata mimi nimewahi kukitembelea kilikuwa na upungufu fulani lakini kama ilivyozungumzwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ni kwamba kimewekwa kwenye bajeti. Hata hivyo, kwa mwaka huu wa fedha tayari Wizara ya Elimu tulikuwa tumeagiza vifaa kwa ajili ya watu wenye ulemavu vya gharama ya shilingi takribani bilioni tatu na tayari vimeshawasili. Kwa hiyo, tutaangalia katika ugawaji na wao waweze kufikiriwa. Ahsante.