Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Risala Said Kabongo

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. RISALA S. KABONGO aliuliza:- Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha Mto Ruaha Mkuu unatiririsha maji yake katika Bwawa la Mtera na Kidatu kwa mwaka mzima kama ilivyokuwa miaka iliyopita?

Supplementary Question 1

MHE. RISALA S. KABONGO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Swali la kwanza, kwa kuwa vyanzo vya maji ya Mto Ruaha Mkuu vinatoka nje ya Bonde la Usangu katika Milima ya Chunya, Mbeya, Mufindi, Mpanga na Kitulo, je, Serikali ina mkakati gani madhubuti wa kushirikisha wananchi katika kutunza vyanzo vya maji visiendelee kuharibika?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Bwawa la Lugola ili kunusuru uhai wa Hifadhi ya Ruaha na Bwawa la Mtera na Kidatu? Ahsante.

Name

Eng. Isack Aloyce Kamwelwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katavi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Spika, kwanza Mheshimiwa Risala amesema Serikali ina mpango gani kuhakikisha kwamba inashirikisha wananchi kwenye utunzaji wa vyanzo vya maji. Katika muundo wa Wizara ya Maji tunayo Idara maalum ambayo inashughulikia utunzaji wa rasilimali za maji.
Mheshimiwa Spika, katika hali hiyo tunashirikisha maeneo ya vijiji, tunaunda kamati ndogo ndogo kwenye maeneo husika ili ziweze kulinda vyanzo vile ambavyo vina manufaa na wao wenyewe. Kwa hiyo, tunafanya ushiriki kupitia kwenye Wilaya, Halmashauri, Mikoa pamoja na vijiji ili kushirikisha hao wananchi.
Mheshimiwa Spika, kuhusu sasa ni lini tutajenga hili Bwawa la Lugoda, sasa hivi tumeshakamilisha usanifu. Sasa hivi Serikali inafanya juhudi ya kuwasiliana na wadau mbalimbali kwa ajili ya kupata fedha ili tuweze kujenga hili Bwawa la Ndembera ambalo litatunza maji na kipindi cha kiangazi maji yatafunguliwa kuhakikisha kwamba Ruaha Mkuu inatiririsha maji wakati wote.