Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ally Abdulla Ally Saleh

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Malindi

Primary Question

MHE. ALLY SALEH ALLY (K.n.y. MHE. MUHAMMED AMOUR MUHAMMED) Aliuliza:- Suala la usalama wa raia na mali zao ni moja ya dhamana ya Jeshi la Polisi nchini; ni muda sasa Zanzibar wananchi wamekuwa wakipigwa, kunyanyaswa na kunyang‟anywa mali zao kunakofanywa na vikosi vya SMZ. Je, nini kauli ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusiana na matukio hayo huko Zanzibar?

Supplementary Question 1

MHE. ALLY SALEH ALLY: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa kweli hii ni standard answer, hata tungefumba macho tu tungejua kwamba jawabu lingekuwa hili. Ni kawaida swali hili limeulizwa hii mara ya tano tangu mimi kuingia Bungeni na Serikali yenye macho, masikio, yenye pumzi, inasema haijui chochote kinachotokea kule Zanzibar. Hili ni jambo la aibu kwa Serikali.
Mheshimiwa Spika, sasa je, kwa sababu hapa mimi mwenyewe nimeleta ripoti za haki za binadamu na nikawapa baadhi ya Mawaziri hapa kuonesha matendo yanayoonekana Zanzibar. Je, Bunge hili kwanza halioni wakati sasa umefika wa kuunda Tume ya Kibunge kuchunguza mambo yanayotokea Zanzibar? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa sababu wananchi wa Zanzibar sasa hawana imani na vituo vya polisi ambako wamekuwa wakiripoti. Je, Mheshimiwa Waziri uko tayari kutoa commitment humu ndani Bungeni leo kwamba tukutane Uwanja wa Amani tarehe ambayo yeye anataka, tumletee wananchi ambao wameonewa, wamenyanyaswa, wamepigwa, wamedhalilishwa, tumuoneshe kwamba watu wapo na ushahidi wa hili Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani akiri, mara ngapi nimemwandikia na hata siku moja hajaja Unguja wala Pemba tukafanya naye kazi kuhusu suala hili? Ahsante.

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, ni kweli Mheshimiwa Mbunge ameshatoa hoja hizo na ameandika, lakini sehemu moja tu anasema Waziri wa Mambo ya Ndani hajaja Unguja ama Pemba. Mimi nimeshafika Unguja na Pemba na…
Mheshimiwa Spika, taratibu za utendaji wa kazi zinafanyika kwa kutumia vikao na baadhi ya Wabunge nilikutana nao, tena Wabunge wa Majimbo mpaka Pemba na Mheshimiwa Khatib ni Mbunge mmojawapo na nilionana naye.
Mheshimiwa Spika, niseme tu kwamba utaratibu wa upokeaji wa malalamiko upo kwa njia zilizo rasmi na hakuna utaratibu wa kuweka parade uwanjani kupokea malalamiko. Kwa sababu vitendo vya aina hiyo ikiwa vimetokea tunapokea malalamiko na kuna taasisi nyingine ambazo zinatakiwa ku-verify kwamba vile vilifanyika.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kwa sababu Mheshimiwa Mbunge ndiyo tunaanza tu Bunge leo, waelekeze watu wako na mimi nitawaelekeza watu wangu wafike na wafikishe hayo malalamiko, halafu verification zifanyike kujua ukweli wa hicho kinachofanyika.