Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto

Sex

Male

Party

ACT

Constituent

Kigoma Mjini

Primary Question

MHE. KABWE Z. R. ZITTO aliuliza:- Mradi wa Maji wa Manispaa ya Kigoma-Ujiji unaogharimu shilingi bilioni 32 ambao unafadhiliwa na Shirika la KFW la Ujerumani na Jumuiya ya Ulaya ulipangwa kukamilika mwezi Machi, 2015:- (a) Je, kwa nini mradi huo umechelewa kukamilika kwa mujibu wa mkataba? (b) Je, Serikali inachukua hatua gani dhidi ya Mkandarasi kwa kuchelewa kukamilisha mradi huo?

Supplementary Question 1

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunafahamu kwamba, moja ya gharama kubwa sana ya miradi ya maji ni gharama za kusukuma maji, pampu za maji na kwa mujibu wa mradi huu tunategemea kutumia pampu za umeme wa mafuta kwa kuweka jenereta na kununua umeme kutoka TANESCO ambapo gharama zitakuwa ni kubwa zaidi kwa wananchi katika kuyalipia hayo maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri haoni kwamba, itakuwa ni jambo la busara na economical kutumia hizi liquidated damages ambazo wamempa Mkandarasi kufunga solar pumps, ili ziweze kupunguza gharama za uendeshaji wa mradi kupelekea wananchi waweze kupata maji kwa gharama nafuu?

Name

Eng. Gerson Hosea Lwenge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli mradi huu kwa usanifu wake tumesanifu kutumia pump kwa kutumia nishati ya umeme. Naomba nipokee ushauri wake kwamba, tuweze kuangalia uwezekano wa kubadilisha. Tukishakuwa tumekabidhiwa huu mradi Serikali tunaweza tukabadilisha sasa pampu zile tutumie solar kwa maana ya kutaka kupunguza gharama za uendeshaji wa mradi ule.

Name

Peter Joseph Serukamba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigoma Kaskazini

Primary Question

MHE. KABWE Z. R. ZITTO aliuliza:- Mradi wa Maji wa Manispaa ya Kigoma-Ujiji unaogharimu shilingi bilioni 32 ambao unafadhiliwa na Shirika la KFW la Ujerumani na Jumuiya ya Ulaya ulipangwa kukamilika mwezi Machi, 2015:- (a) Je, kwa nini mradi huo umechelewa kukamilika kwa mujibu wa mkataba? (b) Je, Serikali inachukua hatua gani dhidi ya Mkandarasi kwa kuchelewa kukamilisha mradi huo?

Supplementary Question 2

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majawabu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, mradi huu wa maji wa Kigoma Mjini utakuwa unazalisha zaidi ya lita milioni 42 kwa siku, Matumizi ya Mji wa Kigoma haitazidi zaidi ya lita milioni 24, wanasema mpaka 25. Mheshimiwa Waziri haoni sasa na hili swali naliuliza mara ya tatu kwamba, mradi huu sasa waongeze vijiji vya jirani ambavyo ni Vijiji vya Mwandiga, Kibingo mpaka Bigabiro pamoja na kwenda Msimba ili na sisi tufaidike kwa sababu, tatizo la maji kwa Jimbo la Kigoma Kaskazini ni kubwa sana?

Name

Eng. Gerson Hosea Lwenge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli mradi huu utazalisha maji mengi zaidi ya lita milioni 42 kwa siku, zaidi ya mahitaji ya wananchi wa Kigoma Mjini. Lengo la Serikali la kuweka mradi huu ni kwamba, lazima tusambaze katika vijiji ambavyo vinazunguka mji ule, ikiwepo na Mwandiga. Kwa hiyo, naomba nimwahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali itazingatia ombi lake na tutahakikisha kwamba, maji haya yanafika mpaka maeneo hayo aliyoyataja.