Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jaku Hashim Ayoub

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Primary Question

MHE. JAKU HASHIM AYOUB aliuliza:- Hivi karibuni tumeshuhudia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizindua Daraja la Kisasa la Kigamboni ambalo limepewa jina la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambaye hakuwahi kuishi Kigamboni; Kwa nini daraja hili halikupewa jina na Rais Mstaafu wa Zanzibar na Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu wa Muungano, Mheshimiwa Aboud Jumbe ambaye ana historia kubwa katika Mji huo kwa kuishi karibu miaka 32.

Supplementary Question 1

MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwanza nakubaliana na Mheshimiwa Naibu Waziri kuwa kutokana na mchango mkubwa wa maendeleo wa Taifa wa Baba Hayati Mwalimu Nyerere ni mkubwa nikiri hivyo, lakini nataka kuweka Hansard sawa. Rais Marehemu Aboud Jumbe ni Rais aliyefungua demokrasia mwanzo Zanzibar ikiwemo Baraza la Wawakilishi la Katiba ya Zanzibar. Lakini kumbukumbu nyingi zinaonyesha Baba Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere anazo ikiwemo Ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa, Dar es Salaam, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa kuitwa jina lake, Mfuko wa Taasisi ya Fedha, kuna barabara hata Zanzibar zipo zinaitwa Baba Nyerere. Leo kweli tunamtendea haki Hayati Aboud Jumbe Mwinyi mtu aliyeishi karibu miaka 32 na kila mmoja Mtanzania anajua aliishi kule Kigamboni.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuteleza siyo kuanguka, kutokuwa na meno siyo uzee, je, Serikali imesema ipo tayari kuchukua mapendekezo yangu na kubadilisha jina hilo? Hilo la kwanza.
Pili, je, kwa nini Serikali haikutafakari mapema na badala yake Serikali inasubiri mapendekezo kutoka kwa Mheshimiwa Mbunge. Lini Serikali ya Jamhuri ya Muungano itawaenzi viongozi wetu kwa kuweka historia katika kumbukumbu ili vizazi vijavyo vikaja kuwa na historia hiyo.

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, hakuna ambaye hatambui michango ya viongozi wetu wa Kitaifa wote, nimwombe tu, bahati nzuri yeye ni Mbunge wa Baraza la Wawakilishi na nina hakika anafahamu kwamba tuna forum kati ya Serikali hizi mbili, tuombe tuzitumie zile forum kama kuna kitu anadhani kina tatizo, tuweze kukijadili na kukirekebisha.
Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba sana kama kuna daraja lingine, kama kuna barabara nyingine, tafadhali wewe tuambie ili tuweze kuangalia uwezekano wa kutumia hilo jina kwa hilo eneo ambalo hata ninyi watu wa Baraza la Wawakilishi mtaridhika nalo.