Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Yahaya Omary Massare

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni Magharibi

Primary Question

MHE. YAHAYA O. MASSARE aliuliza:- Barabara ya Mkiwa – Rungwa - Makongorosi ni ya udongo na nyakati za mvua barabara hiyo inaharibika sana kiasi cha kutopitika kabisa:- Je, Serikali ina Mpango gani wa kuitengeneza barabara hiyo kwa lami ili kuwaondelea kero wananchi wa Jimbo la Manyoni Magharibi hususan wa Kata za Mwamagembe, Rungwa na Kijiji cha Kitanula.

Supplementary Question 1

MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Kwa kuwa katika barabara hii korofi kipindi chake cha kuharibika sasa kimekaribia, kipindi cha mvua ambacho katika maeneo ya Lulanga, Itagata, Ukimbu, Mitundu, Kiombo, Mwamaluku, Mwamagembe, Kintanula hadi Rungwa udongo huo aliousema ni mbaya na ukarabati uliofanyika kipindi cha nyuma ulikuwa haukidhi kiwango. Je, sasa Serikali iko tayari kufanya marekebisho ya kutosha katika kipindi hiki kabla mvua hazijaanza?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; katika ujenzi wa kipande hiki cha kilometa 57 ambacho Meshimiwa Naibu Waziri amekisemea hapa, watakapoanza wanatarajia ni muda gani utachukua kukamilika? Maana yake wananchi wanahamu kubwa ya kuona barabara ya lami katika kipande hiki nikiwemo mimi Mbunge wao.
Mhesshimiwa Naibu Spika, ahsante.

Name

Eng. Edwin Amandus Ngonyani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tu nimjulishe Mheshimiwa Mbunge kwamba, baada ya Bunge hili nitakuwa na safari ya kuipitia barabara hii. Nitamjulisha Mheshimiwa Mbunge tarehe kamili nitakapokuwa katika eneo lake ili tusaidiane kutambua kwa karibu zaidi na kwa macho siyo kuandikiwa tu, hatimaye tuhakikishe tunaposimamia hatua za marekebisho ambazo Mheshimiwa Mbunge anazihitaji tuweze kuzisimamia vizuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu lini tutakamilisha, nimwombe Mheshimiwa Mbunge ajue dhamira ya Serikali hii ya kuikamilisha hii barabara, aone kama ambavyo tumejibu katika swali la msingi maeneo ambayo tayari tumeyakamilisha na tupo katika kuendelea kukamilisha maeneo yaliyobaki. Naomba atuamini, kusema ni lini huwa naogopa sana kwa kazi hizi za ujenzi ambazo zina process, lazima upate hela na hatimaye ujihakikishie kipande gani kinakamilika kwa wakati gani. Naomba aniwie radhi kwamba hiyo kazi ya kusema lini hasa siyo rahisi sana. Kikubwa tuna dhamira ya dhati na tutakamilisha kujenga hii barabara kama ambavyo kwenye Ilani imeeleza. Ahsante.