Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Munira Mustafa Khatib

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MUNIRA MUSTAFA KHATIBU aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuanzisha vituo maalum vya kulelea watoto wanaozaliwa kabla ya wakati kuliko ilivyo sasa ambapo huchanganywa na watoto wenye matatizo mbalimbali?

Supplementary Question 1

MHE. MUNIRA MUSTAFA KHATIBU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Kwanza, nakushukuru Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa majibu yake mazuri ambayo amenijibu, lakini napenda kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza. Je, ni utaratibu gani uliotumika kugawa hivi vifaa katika hospitali zetu za wilaya na mikoa kwa sababu vifaa hivi ndani ya hospitali zetu za wilaya na mikoa havionekani?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, je, ni utaratibu gani unaotumika kuwapa elimu akinamama wajawazito kuweza kuwalea watoto hawa?

Name

Dr. Hamisi Andrea Kigwangalla

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI, WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza Kangaroo Mother Care haihitaji vifaa vyovyote vile, kwa sababu ni huduma ambayo inatolewa na aidha mzazi mama, baba, ama mtoa huduma yeyote yule ambaye atakuwa amechaguliwa na familia kutoa huduma hiyo. Huduma hii inahusisha kumchukua mtoto kumweka kifuani ngozi kwa ngozi na mzazi huyo, mara nyingi inakuwa ni mama. Kwa maana hiyo, hakuna vifaa vinavyohitajika pale zaidi ya mashuka na mablanketi ambayo yanagawanywa kwenye hospitali zote nchini kwa utaratibu wa kawaida wa kila siku.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kwa sasa kupitia Wizara ya Afya ina encourage zaidi kutoa huduma kwa kutumia njia hii ya Kangaroo Mother Care na ndiyo maana hatuwekezi sana kwenye kujenga vituo maalum pembeni kwa ajili ya kuwatenga watoto na wazazi wao, kwa sababu imeonekana wakikaa na wazazi wao wanajengwa afya zao kisaikolojia zaidi.