Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Flatei Gregory Massay

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Vijijini

Primary Question

MHE. FLATEI G. MASSAY aliuliza:- Hospitali ya KKKT Hydom ilipanda hadhi kuwa Hospitali ya Mkoa muda mrefu, sasa inahudumia Mikoa ya Manyara, Shinyanga, Singida, Arusha na Simiyu:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuipandisha hadhi ili iwe Hospitali ya Kanda kuiwezesha kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi?

Supplementary Question 1

MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri amefika katika hospitali ya Hydom, lakini nina maswali mawili madogo ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa Naibu Waziri amekiri kwamba hospitali hii imepandishwa hadhi miaka sita toka 2010 hadi leo ya kuwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na haijapata hata siku moja ile haki ya kibajeti ya hospitali ya Mkoa. Je, sasa ni lini hospitali hii itatengewa bajeti ili ifanane na hospitali zote za Rufaa za Mikoa ya Tanzania?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa kwenye majibu ya msingi amesema hospitali hii ina tatizo la miundombinu na watumishi. Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kuijengea uwezo na kuipatia watumishi ili hospitali ya Haydom iweze kutoa huduma kwa sababu na yeye amekiri kwamba inafikika na maeneo ya jirani na mikoa hii?

Name

Dr. Hamisi Andrea Kigwangalla

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Flatei Massay kwa ufuatiliaji anaoufanya kiasi kwamba amenilazimisha kufika kwenye hospitali hii katika ziara zangu mara mbili toka nimeteuliwa katika nafasi hii. Katika mara zote nimefika na kutatua changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikiikabili hospitali hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukweli ni kwamba, pamoja na kwamba hospitali hii ingependa iwe Hospitali ya Rufaa ya Kanda bado haijakidhi vigezo. Pili, kuteuliwa kuwa hospitali ya ngazi ya Kanda hakuifanyi hospitali kudai haki ya kupewa fedha kibajeti wakati haimilikiwi na Serikali. Serikali inashirikiana na mashirika ya hiyari kama KKKT kutoa huduma kwa wananchi kwa kuwawezesha kupata michango ya health basket fund pamoja na watumishi ambao wanapelekwa by secondment na Serikali kwenye hospitali husika. Kwa sasa, Mkoa wa Manyara una hospitali yake ya rufaa ya mkoa na Serikali inaijengea uwezo hospitali hii ili iweze kutoa huduma ambazo zinaendana na hadhi ya hospitali ya rufaa ya mkoa.