Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Cecilia Daniel Paresso

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CECILIA D. PARESSO (K.n.y MHE. GODBLESS J. LEMA) aliuliza:- Mahitaji ya tairi za magari katika Mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla ni makubwa. Mpango wa Serikali kufufua kiwanda cha tairi cha General Tyre unaonekana kwenda taratibu:- (a) Je, ni lini Serikali itatambua umuhimu wa kiwanda hicho kuanza uzalishaji mapema; (b) Wapo baadhi ya waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda hicho bado hawajalipwa mafao tangu kiwanda kifungwe: Je, Serikali ina mpango gani wa kuwahakikisha wafanyakazi hao wanalipwa stahili zao?

Supplementary Question 1

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba niulize maswali madogo mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa, umuhimu wa kiwanda hiki cha matairi unajulikana na uwepo wa kiwanda hiki kufufuliwa katika Mkoa wa Arusha utaongeza ajira, lakini katika mwaka huu wa fedha Serikali imetenga shilingi bilioni 60, mpaka tunapoongea imetolewa shilingi bilioni mbili tu. Je, kwa Serikali hii ambayo imefilisika kuna dhamira ya kweli kufufua kiwanda hiki?
Swali la pili; kuna wafanyakazi ambao bado wanakidai kiwanda hiki na madai yao wameshayafikisha Hazina, lakini mpaka leo hawajalipwa. Je, ni lini sasa madai haya ya wafanyakazi yatalipwa?

Name

Charles John Mwijage

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba Kaskazini

Answer

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na lile gumu la madai ya wafanyakazi. Mheshimiwa Mbunge naomba nakala ya madai iliyopelekwa kwa Treasury Registrar, nipewe nakala hiyo, mimi nitafuatilia. Naomba Mheshimiwa Mbunge anifuatilie mimi na mimi nimfuatilie Treasury Registrar.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza juu ya dhamira ya kweli, Serikali hii ina dhamira ya kweli na nitumie fursa hii, kwamba Tanzania kuna soko la matairi siyo habari mpya, kwamba sisi ni sehemu ya Afrika Mashariki, it is not the news, kwamba sisi tuko SADC siyo tatizo, tumeelekezwa katika Ilani ya Chama chetu na Mpango wa Pili wa Miaka Mitano General Tyre ifufuke.
Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue fursa hii kama kuna mtu yeyote ana mwekezaji, anataka kujenga kiwanda mimi nitahakikisha nitajenga kiwanda, Mheshimiwa Rajab Adadi na Mheshimiwa Stephen Ngonyani (Majimarefu) wamekuwa wakinifuatilia, fursa ipo, sisi kazi yetu ni kuweka mazingira wezeshi, kupiga sound ili kusudi wawekezaji waje wawekeze, Serikali haitajenga kiwanda inatengeneza mazingira wezeshi.