Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Zuberi Mohamedi Kuchauka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Liwale

Primary Question

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza:- (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha vijiji vya Mlembwe, Kimambi, Lilombe, Mirui, Mpigamiti, Kikulyungu na Mtungunyu vinapata miradi ya mawasiliano ya simu za mkononi? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuimarisha usikivu hafifu wa matangazo ya Redio Tanzania (TBC – Taifa) katika Wilaya ya Liwale?

Supplementary Question 1

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, natoa shukrani zangu kwa Mheshimiwa Waziri kwa majibu ya kutia matumaini. Lakini nataka ieleweke kwamba Wilaya ile ya Liwale ipo mbali sana na makao makuu ya Mkoa, Wilaya ya Liwale haina usafiri, haina barabara za kutosha yaani za kuaminika, Wilaya ya Liwale haina mtandao wa simu unaoaminika, Wilaya ya Liwale haina usikivu wa redio. Sasa muone jinsi Wilaya hii ilivyo kisiwani, hawa ni miongoni mwa walipa kodi wa nchi hii, sijui kama kodi zao watanufaika nazo vipi? Nashukuru kwa jibu la kwanza nimepata timeframe na mimi nitafuatilia kuhakikisha hii timeframe inafikiwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kwa swali la pili napata wasiwasi, nimepata tu majibu ya moja kwa moja. Nahitaji kujua ni lini Redio Tanzania itasikika Liwale? Hapa nimepewa tu majibu ya jumla jumla. Mwisho kabisa hapa amesema kwamba mpango wa muda mrefu sasa hata huo mpango wa muda mfupi nao haujatajwa, huo ni wa lini? Naomba nipatiwe majibu.

Name

Nape Moses Nnauye

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtama

Answer

vipi? Nashukuru kwa jibu la kwanza nimepata timeframe na mimi nitafuatilia kuhakikisha hii timeframe inafikiwa.