Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Neema William Mgaya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NEEMA W. MGAYA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itahakikisha wakulima wanapata pembejeo za kilimo kama mbolea kwa wakati kwa kuwa tatizo hilo limekuwa sugu?

Supplementary Question 1

MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri. Kwa kuwa hatuna muda nitauliza swali moja tu la nyongeza na swali langu liko hivi. Kwa kuwa, kumekuwa na mlolongo mrefu wa upatikanaji wa pembejeo za kilimo kwa wakulima.
Je, Serikali haioni sasa kuna umuhimu wa kutafuta njia mbadala ili kufupisha mlolongo huo?

Name

William Tate Olenasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. Serikali iko kwenye mpango tayari wa kupitia mfumo wa kutoa pembejeo ili kuleta mfumo ambao utaleta ufanisi zaidi katika ugawaji wa pembejeo ambao sisi tunaamini kwamba siyo tu kwamba, utarahisisha upatikanaji wa pembejeo kwa wakati, lakini vilevile kwa bei nafuu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni kama mnavyofahamu tumekutana na Wabunge wote wanaotoka maeneo wanayolima mazao muhimu ili kupata mawazo yao ya namna ya kuboresha mfumo huu. Nawaahidi kwamba, katika bajeti inayokuja, Serikali inakuja na mapendekezo ya mpango mpya kabisa ambao utaondoa hii kero na changamoto, ili isiwepo tena. Nashukuru sana.