Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Hafidh Ali Tahir

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dimani

Primary Question

MHE. HAFIDH ALI TAHIR aliuliza:- Chaguzi zetu zimekuwa zikikumbwa na matatizo mengi yanayosababisha upotevu wa fedha nyingi za Taifa jambo linaloweza kuepukika kwa faida ya Watanzania mathalani inapotokea mshindi wa uchaguzi wa Jimbo wa chama fulani amefariki hurudiwa badala ya nafasi hiyo kuchukuliwa na mshindi wa pili ndani ya chama hicho. (a) Je, Serikali haioni umuhimu wa kuweka utaratibu kuwa pindi mshindi wa jimbo kupitia chama fulani anapofariki mshindi wa pili ndani ya chama apewe nafasi aliyoiacha marehemu badala ya kurudia uchaguzi? (b) Je, Serikali haioni kuwa ni wakati muafaka kuondoa utaratibu wa kusimamisha uchaguzi mkuu wakati mgombea anapofariki?

Supplementary Question 1

MHE. HAFIDH ALI TAHIR: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimshukuru sana Naibu Waziri kwa majibu yake lakini wakati akijibu swali langu alikuwa ameweka wazi kwamba sheria ya uchaguzi inaweza kufanyiwa marekebisho kulingana na wakati uliopo, swali langu kwamba hahisi kwamba sasa wakati wenyewe uliopo ndio huu, na tunapofika mwaka 2020 sheria hii tukaifanyia marekebisho, anasemaje?
Swali la pili, kwa sababu Waziri Mkuu yeye mwenyewe ni Mbunge wa kuchaguliwa na anahisi na anajua ugumu wa gharama katika jimbo, hivi Naibu Waziri si lazima anipe kwa ukamilifu lakini anachoweza kuliambia Bunge hili kiasi ambacho anafikiria hutumika katika kurudia uchaguzi katika majimbo yetu? Ahsante.

Name

Dr. Abdallah Saleh Possi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, WATU WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kuhusu suala la kufanyia marekebisho swali hili lilikuwa lina vifungu (a) na (b) na nilijibu katika kile cha (b) kuhusiana na suala la kusimamisha uchaguzi pale anapofariki mgombea, of course hilo liko wazi lakini mwisho wa siku tunaobadilisha sheria ni sisi kama inaona inafaa na wadau watapendekeza basi hilo suala linaweza likaletwa Bungeni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kama mabadiliko hayo yalikuwa yanahusiana na kubadilisha ule mfumo wa uchaguzi kwamba akifariki mgombea ubunge basi yule aliyekuwa mshindi wa pili katika chama husika anachukua nafasi hiyo, hili si jambo rahisi sana na labda niseme tu ukiangalia system za uchaguzi duniani zipo takribani 23 sasa kwa nini nchi moja wakaamua kupigia chama, kwingine wakaamua kupigia mgombea, kwingine wakaamua kupigia orodha ya wagombea iliyofungwa ya chama, kwingine wakaamua kupigia orodha ya wagombea wa chama iliyokuwa wazi, kwingine wakaamua kuchanganya ni swali gumu kidogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo niseme tu demokrasia yetu inakuwa na kubadilika kwa demokrasia, kubadilika kwa mifumo ya uchaguzi kwa namna moja au nyingine ni sehemu ya historia basi muda utakapofika utatoa majibu sahihi.