Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Rwegasira Mukasa Oscar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Biharamulo Magharibi

Primary Question

MHE. OSCAR R. MUKASA aliuliza:- Biharamulo ni moja ya Wilaya za Mkoa wa Kagera zilizoathirika sana na ugonjwa wa mnyauko wa migomba na hivyo ustawi wa zao hilo kuu la chakula upo mashakani. Je, Serikali inatoa kauli gani isiyo nyepesi na inayolingana na uzito wa suala hili?

Supplementary Question 1

MHE. OSCAR R. MUKASA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri.
Kwanza ni amani yangu kwamba wataalamu waliopelekwa kutoa ushauri wa kupelekwa Wilayani Chato ila wamepeleka Wilayani Biharamulo.
Pili maelezo kidogo tatizo hili limekuwepo kwa miaka mingi na tumekuwa tunapata majibu mara nyingi kutoka Serikalini ambayo kwa kweli hayajaweza kukidhi kulingana na ukubwa wa tatizo. Tulisikia swali la kisera kuelekea kwa Waziri Mkuu mwezi wa saba likapelekea kiti chako Mheshimiwa Naibu Spika kutoa maelekezo kwamba Serikali ichukue hatua na ilete majibu hapa.
Sasa swali langu kwa sababu hali halisi inaonesha kabisa kwamba tatizo hili ili likabiliwe kuna mambo matatu lazima yafanyike la kwanza utafiti ili kuja tatizo ni nini ambalo tayari...
MHE. OSCAR R. MUKASA: Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu je, Mheshimiwa Naibu Waziri uko tayari kufanya kikao maalum na Wabunge wa Mkoa wa Kagera ili tuone namna gani tunaweka mikakati ya kutafuta utashi wa kisiasa wa kukabili tatizo hili, lakini namna ya kutafuta na kuwashirikisha wadau wengine wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi na hata private sector ndani ya Tanzania ili tukabiliane na tatizo hili? Kama uko tayari, upo tayari kwa muda wa karibuni, muda wa kati au muda wa mbali?

Name

William Tate Olenasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nilipotaja Chato nilisahau Biharamulo, lakini mimi ndiyo sijasoma kwa hiyo nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Biharamulo nayo imo.
Kuhusu ombi lake la kufanya mkutano, tayari nimeshawasiliana na Mheshimiwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi na ameahidi kwamba tukitoka kwenye Bunge hili atafanya mkutano na Wabunge wanaotoka Mkoa wa Mwanza vilevile Mkoa wa Kagera ili kuangalia namna ya kuweza kushughulikia tatizo hili, kwa hiyo kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge tayari tumepokea na tutafanya haraka tuweze kukutana nao. (Makofi)