Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Eng. James Fransis Mbatia

Sex

Male

Party

NCCR-Mageuzi

Constituent

Vunjo

Primary Question

MHE. JAMES F. MBATIA (K.n.y. MHE ANTONY C. KOMU) aliuliza:- Tarehe 13/8/2012 Halmashauri ya Wilaya ya Moshi ilitangaza zabuni Tenda Na. LGA/046/2011/2012/RWSSP/1 katika gazeti la Mwananchi. Tenda hiyo ilihusu mradi wa mfumo wa kusambaza maji na ungehusisha Vijiji vya Mande na Tella katika Kata ya Oldmoshi Magharibi. Hadi sasa mradi huo haujaanza pamoja na ufuatiliaji wa karibu wa Diwani na Kamati za Maji za Vijiji vya Tella na Mande hawakufanikiwa kupata majibu juu ya mradi tajwa. Je, ni lini Serikali itaanza kujenga mradi huo muhimu kwa wananchi?

Supplementary Question 1

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Chanzo cha maji Masokeni kuimarishwa kwa shilingi milioni 759 na miundombinu ya kuhakikisha Vijiji vya Mande na Tella katika Jimbo la Moshi Vijijini ni fedha kidogo kwa kuwa eneo lenyewe ni kubwa, mahitaji ni makubwa. Serikali inaji-commit vipi kuhakikisha kwamba pamoja na fedha hizi watatafuta chanzo kingine cha fedha ili mradi huu ukamilike kama walivyoahidi hapa? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Vijijini, Kata nyingine za Kirua Kusini, Mamba Kusini, Mwika Kusini, Kahe Mashariki, Kahe Magharibi pamoja na Makuyuni ambayo ni Mji mdogo wa Himo ambao unapanuka kwa kasi kubwa tatizo la maji ni kubwa sana na Kata ya Mamba Kusini imebidi Diwani aanze kufanya harambee... (Makofi)
MHE. JAMES F. MBATIA: Ndiyo nauliza swali, Serikali inaji-commit vipi kwenye maeneo haya mengine niliyoyataja ambayo maji ni muhimu kwa uhai wao ili waweze kupata maisha endelevu kama raia wengine wa Jamhuri ya Muungano? (Makofi)

Name

Eng. Gerson Hosea Lwenge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze Naibu Waziri kwa majibu mazuri aliyoyatoa kwamba kwanza walitangaza tenda, halafu mradi ule haujaanza. Hata hivyo, tumeshatoa maelekezo kwa Halmashauri zote ile miradi ambayo haikuanza kwa sababu ya ukosefu wa fedha kwamba miradi hii ndio viwe vipaumbele kwa awamu hii tunavyoanza katika utekelezaji wa bajeti ya 2016/2017, hayo ndiyo maelekezo tuliyoyatoa. Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kwamba fedha ni kidogo, ni kweli shilingi milioni 759 haiwezi kumaliza mradi kwa mara moja, lakini ni fedha ambayo unaweza ukatangaza ukampa advance mkandarasi akaanza kujenga. Sasa hivi tunazo fedha za Mfuko wa Maji ambazo tunapeleka kukwamua miradi yote inayoendelea. Kwa hiyo, naomba sana Halmashauri wakaanze kazi fedha hizi zinatosha kupeleka Vijiji vya Tella na Mande. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu yale maeneo mengine ambayo umesema yana matatizo makubwa. Nayo pia tumetoa maelekezo kwamba kila Halmashauri iweke mpango wake katika kutekeleza awamu ya pili ya program ya maji kwamba tukimaliza vijiji kadhaa tunaendelea na vijiji vingine ili tufikishe ile azma kwamba Serikali inataka tukifika mwaka 2020 tuwe na 85% wananchi wanaokaa Vijijini wanapata maji na wanaokaa mijini wanapata kwa 95%. Kwa hiyo, tumeshatoa maelekezo usiwe na wasiwasi Mheshimiwa Mbatia tutakwenda kupeleka maji katika maeneo yote kulingana na namna tulivyopanga bajeti. (Makofi)

Name

Saed Ahmed Kubenea

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Ubungo

Primary Question

MHE. JAMES F. MBATIA (K.n.y. MHE ANTONY C. KOMU) aliuliza:- Tarehe 13/8/2012 Halmashauri ya Wilaya ya Moshi ilitangaza zabuni Tenda Na. LGA/046/2011/2012/RWSSP/1 katika gazeti la Mwananchi. Tenda hiyo ilihusu mradi wa mfumo wa kusambaza maji na ungehusisha Vijiji vya Mande na Tella katika Kata ya Oldmoshi Magharibi. Hadi sasa mradi huo haujaanza pamoja na ufuatiliaji wa karibu wa Diwani na Kamati za Maji za Vijiji vya Tella na Mande hawakufanikiwa kupata majibu juu ya mradi tajwa. Je, ni lini Serikali itaanza kujenga mradi huo muhimu kwa wananchi?

Supplementary Question 2

MHE. SAED A. KUBENEA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Matatizo yaliyopo katika Jimbo la Moshi Vijijini yanafanana na matatizo yaliyopo katika Jimbo la Ubungo maeneo ya Kilungule, Kimara Baruti, Korogwe na Golani, Kata ya Kimara pamoja na Makoka, Kajima na Nova Kata ya Makuburi. Je, Serikali ni lini itawapatia maji wananchi wa maeneo hayo? Ahsante sana.

Name

Eng. Gerson Hosea Lwenge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, maeneo ya Ubungo maeneo mengi tunategemea yatapata maji baada ya kukamilisha huu mradi wa Ruvu Juu ambao tayari umeshakamilika. Tatizo lililopo ni kwamba umeme uliopo pale Ruvu Darajani ni mdogo tuna pump kubwa sana ya kuleta maji Dar es Salaam; tumeshaanza kuvuta line ya umeme kutoka Chalinze kuleta pale. Tutakapomaliza line ya umeme maeneo yote ya Ubungo yale yatapata maji kutoka Ruvu Juu. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge asiwe na shaka.