Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Susanne Peter Maselle

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SUSANNE P. MASELLE aliuliza:- (a) Je, Serikali imechukua juhudi gani za makusudi kudhibiti vitendo vya kubambikizia watu kesi vinavyofanywa na baadhi ya askari wasiokuwa na maadili? (b) Je, Serikali itakuwa tayari kuanzisha kitengo cha siri ndani ya Jeshi la Polisi kitakachoshughulikia adha hii?

Supplementary Question 1

MHE. SUSANNE P. MASELLE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi hii nami niweze kuuliza swali moja la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika,Serikali inatoa kauli gani kwa Jeshi la Polisi kupitia askari wasio waadilifu wanaokamata watu hasa viongozi na wafuasi wa UKAWA na kuwaweka mahabusu kwa zaidi ya saa 24 bila kuwapeleka mahakamani wakijua kwamba wanavunja sheria kwa kuwabambikizia kesi za uchochezi na CyberCrime? Ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, Jeshi la Polisi linapokamata watu huwa haliangalii itikadi zao na linapowafikisha watu mahakamani haliwaulizi kadi ya chama alichonacho, bali Jeshi la Polisi hukamata watu kufuatana na kosa alilofanya. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kama ilivyo kwa Watanzania wengine, akishakamatwa, kuna hatua ambazo zinafanyika na baada ya hapo anafikishwa mahakamani. Nakushukuru sana. (Makofi)