Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Pauline Philipo Gekul

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Babati Mjini

Primary Question

MHE. PAULINE P. GEKUL (K.n.y. MHE. ZUBEDA H. SAKURU) aliuliza:- Kuwepo na matukio ya vifo visivyokuwa vya lazima kunatokana na kutokuwepo kwa motisha kwa madaktari na wauguzi kwa kulipwa viwango duni vya mishahara na kutolipwa posho zao kwa wakati. Je, Serikali inakabiliana vipi na changamoto ya maslahi kwa watumishi wa sekta hii muhimu?

Supplementary Question 1

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Naomba niulize maswali mawili ya nyongeza.
Kwa kuwa pamoja na mishahara ya watumishi hawa wa sekta ya afya, Serikali ilikuwa ikitoa motisha mbalimbali ikiwemo on call allowance kwa wauguzi wetu; lakini hadi hivi tunavyoongea Serikali haipeleki pesa hizi kwa wakati; na nitoe mfano kwa Hospitali yangu ya Mrara katika Jimbo la Babati Mjini, tangu mwezi wa pili wauguzi wale katika hospitali ile tangu mwezi wa pili hawajalipwa fedha hizo.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nifahamu, ni kwa nini Serikali haipeleki fedha hizi kwa wakati kama ilivyoahidi?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa katika bajeti iliyopita OC katika Halmashauri zetu na katika hospitali zetu zilipunguzwa kwa zaidi ya asilimia 60; nitoe mfano wa hospitali yangu ya Mrara, ilikuwa inapokea OC ya shilingi milioni 154 lakini ikapunguzwa hadi shilingi milioni 46 kwa mwaka na hizi fedha sasa zilipe likizo za watumishi, maji na umeme.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nifahamu kauli ya Serikali, ni kwa nini fedha hizi zimepunguzwa ilhali mambo haya sasa yamekwama? Mfano sisi, zaidi ya shilingi milioni 10 hospitali inadaiwa, imeshindwa kulipa BAWASA bili ya maji. Serikali iko tayari kufikiria kuhusu uamuzi huu wa kupunguza OC katika hospitali zetu za Wilaya ili waweze kuziendesha hospitali hizi? (Makofi)

Name

Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Pauline Gekul, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Eeh, unisamehe Mheshimiwa Pauline Gekul, ni Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini, ulitokea Viti Maalum, uniwie radhi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na suala lake la kwanza kwamba ni kwa nini Serikali haipeleki kwa wakati posho mbalimbali hususan ya on call allowance, nimejaribu kufanya ziara katika maeneo mbalimbali, ni kweli posho hii imekuwa ikichelewa, lakini nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba itaendelea kutolewa kwa wakati kwa kadri hali ya uchumi itakavyoendelea kuimarika kwa sababu fedha hizo tayari zilishapangwa katika bajeti, kwa hiyo, zitatolewa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na OC kupunguzwa, haijapunguzwa kwenye OC za Hospitali ya Mrara peke yake, ukiangalia nchi nzima fedha za matumizi mengineyo zilipunguzwa na wote tunajua kabisa, tulikuwa na malengo ya aina gani kama nchi, asilimia zaidi ya 40 imepelekwa katika miradi ya maendeleo.
Mheshimiwa Naibu Spika, nawaomba watumishi waendelee kuvuta subira, tutakapoenda katika mid year review, siwezi kulisemea hili kwa Wizara ya Fedha, tunajua kabisa kila mwaka mwezi Januari au Februari huwa kuna mid term year review. Kwa hiyo, hilo niwaachie wao, naamini itakapofika wakati huo, wataona ni maeneo gani yanayoweza kufanyiwa maboresho ili kuweza kuendana na wakati. Nakushukuru.