Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Hafidh Ali Tahir

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dimani

Primary Question

MHE. HAFIDH ALI TAHIR (K.n.y. MHE. HAMADI SALIM MAALIM) aliuliza:- Jeshi la Polisi ni chombo muhimu kinacholinda usalama wa raia na mali zao. Askari hawa wanapomaliza mafunzo yao kwa ngazi mbalimbali kama vile Sajenti, Staff Sajenti, Meja na nyingine, hucheleweshwa sana kulipwa maslahi yanayoendana na vyeo vyao:- Je, ni kwa nini Askari hao hawalipwi kwa wakati?

Supplementary Question 1

MHE. HAFIDH ALI TAHIR: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, ucheleweshaji wa malipo ya Askari hawa wanapomaliza mafunzo Mheshimiwa Waziri haoni kama yanasababisha suala la rushwa ili Askari hao wapate maslahi yao?
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini la pili, inakuwaje Serikali inachelewesha maslahi ya Askari hao wenye vyeo wakati wanajua kwamba Askari wamekwenda mafunzoni na watamaliza mafunzo hayo muda fulani. Kwa nini wasiwatengee mapema ili tatizo hili liondoke?

Name

William Tate Olenasha

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu kwamba ucheleweshaji unaleta mambo ya rushwa, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba utaratibu wa kurekebisha changamoto hizi uko wazi kwa hiyo haimlazimishi Askari yeyote ambaye anadai malimbikizo ya mishahara yake kutoa rushwa. Serikali inatambua kuhusu deni hili na tayari katika bajeti iliyopita ya Wizara ya Mambo ya Ndani imetengwa fedha kwa ajili ya kulipa malimbizkizo haya. Kwa hiyo, niwahakikishie tu Askari ambao wanadai malimbikizo kwamba wasubiri kwa sababu malimbikizo hayo yatalipwa haraka iwezekanavyo katika bajeti inayokuja.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali lake la pili kwamba kwa nini ucheleweshaji unatokea, nimfahamishe Mheshimiwa Mbunge kwamba ucheleweshaji uliotokea umetokea kwa sababu za kitaalam kwamba wakati Maaskari wameenda kwenye mafunzo mwaka 2013 kibali cha kwenda mafunzo pamoja na ikama ilikuwa imeombwa lakini kwa bahati mbaya ikawa imechelewa na Askari wakawa wameenda kwenye mafunzo na walipotoka kwenye mafunzo wakapandishwa vyeo wakati bado ikama haijatoka.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge pamoja na Askari ambao wameathirika kuwa ikama hiyo imeshatoka sasa. Kwa hiyo, malipo yao yako njiani, wafuate tu taratibu ambazo zinafahamika ambapo katika Jeshi la Polisi ni lazima wawasilishe madai yao ya salary arrears kwenye Kamandi ya Maslahi ya Makao Makuu na watapatiwa fedha zao bila kuchelewa. Nashukuru.