Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Catherine Valentine Magige

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CATHERINE V. MAGIGE (K.n.y. MHE. GODBLESS J. LEMA) aliuliza:- Hivi karibuni Mheshimiwa Rais ameamuru Wakuu wa Mikoa kuwakamata na kuwaweka mahabusu vijana watakaokutwa wanacheza pool table na draft mitaani kama ishara ya mizaha katika nguvukazi:- (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kutengeneza ajira ili vijana waweze kuajiriwa na kuepuka adhabu hiyo itakayotekelezwa na Wakuu wa Mikoa? (b) Ni dhahiri kwamba Taifa letu linapita katika adhabu kubwa ya umaskini. Je, Serikali haioni kwamba Taifa linaweza kuingia katika vurugu kati ya vijana wasiokuwa na ajira na Jeshi la Polisi?

Supplementary Question 1

MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa kuwa vijana hawa wa Arusha ambao wamekuwa wakitumiwa na Mbunge huyu huyu kuandamana hawana ajira lakini inapofikia wakati wa kuwasilisha matatizo yao Bungeni Mbunge huyu akatolewa kwa ajili ya utovu wa nidhamu, je, Serikali haioni sasa ni wakati wa kuwasikitikia vijana wa Arusha kwa kuwapatia mafunzo na mitaji ili waendelee kutoa kura kwa Serikali hii sikivu ya Chama cha Mapinduzi?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa nataka niwaondoe hofu vijana wa Arusha. Pamoja na kwamba wamekosa kisemeo chao humu ndani kwa maana yule ambaye walimpa dhamana hayupo kwa ajili ya kuwasilisha matatizo yao lakini Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kuwajali vijana bila kubagua. Sisi katika utekelezaji wa majukumu yetu mbalimbali tutahakikisha vijana wa Arusha kama vijana wa maeneo mengine na wenyewe wanapata fursa za elimu ya ujasiriamali, mikopo na mitaji. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi binafsi nimeshafika pale Arusha na nimeshakutana na vijana wa SACCOS katika soko la Korokoroni na nimewaahidi kwamba nitarudi kwa ajili ya kuendelea kuwasaidia katika kupata mitaji na mikopo. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge nikuondoe tu wasiwasi ya kwamba kama Serikali vijana hawa tutaendelea kuwaangalia.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WATU WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa, naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri lakini naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Catherine kuwa kisemeo kipya cha vijana wa Arusha na hasa kuendelea kuwa daraja la kutu-link kati ya Serikali na vijana wa Arusha ili waweze kufanikiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Ibara ya 25 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasisitiza sana kwamba kazi ndiyo kipimo cha utu wa kila Mtanzania. Kifungu cha 28(b) cha Sheria ya Mwenendo ya Mashauri ya Jinai na chenyewe kinasisitiza sana masuala ya kila Mtanzania kuwajibika na apimwe kwa kuwajibika na aweze kukidhi riziki zake kwa kuwajibika yeye mwenyewe.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba niwaambie Waheshimiwa Wabunge, kama kuna Mheshimiwa Mbunge anawatumia vijana na kuwahamasisha wasifanye kazi anaenda kinyume na Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hivyo basi kukiuka misingi yote ya utawala bora. Kwa hiyo, naomba kuwaambia Waheshimiwa Wabunge na vijana wote maelekezo yaliyotolewa na Mheshimiwa Rais wetu ni sahihi. Vijana wanaweza kucheza pool katika saa ambazo si za kazi lakini saa za kazi kila mtu awajibike ili kuweza kupata riziki yake na kuweza kujenga uchumi wa nchi yetu ya Tanzania.

Name

Dr. Faustine Engelbert Ndugulile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigamboni

Primary Question

MHE. CATHERINE V. MAGIGE (K.n.y. MHE. GODBLESS J. LEMA) aliuliza:- Hivi karibuni Mheshimiwa Rais ameamuru Wakuu wa Mikoa kuwakamata na kuwaweka mahabusu vijana watakaokutwa wanacheza pool table na draft mitaani kama ishara ya mizaha katika nguvukazi:- (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kutengeneza ajira ili vijana waweze kuajiriwa na kuepuka adhabu hiyo itakayotekelezwa na Wakuu wa Mikoa? (b) Ni dhahiri kwamba Taifa letu linapita katika adhabu kubwa ya umaskini. Je, Serikali haioni kwamba Taifa linaweza kuingia katika vurugu kati ya vijana wasiokuwa na ajira na Jeshi la Polisi?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kunipatia fursa ya kuuliza swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa changamoto ya ajira imekuwa kubwa sana nchini hususan kwa upande wa vijana na kwa kuwa Halmashauri zimekuwa zinatenga asilimia 10 kwa ajili ya kukopesha akina mama na vijana lakini katika baadhi ya Halmashauri kumekuwa na changamoto kubwa. Je, Serikali haioni sasa ni muda muafaka kutenga kati ya asilimia 10 - 30 ya tenda zote za Serikali ili kuweza kuwapatia fursa za kujiajiri vijana?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli imekuwepo asilimia 5 ya mikopo katika kila Halmashauri kwa ajili ya vikundi vya akina mama na vijana na ambapo kwa kiasi kikubwa vijana na akina mama wengi wamekuwa wakinufaika kupitia mfuko huu. Pia kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM imeelezwa wazi kabisa kwamba moja kati ya mipango ambayo tunatazamia kutekeleza mwaka huu ni kuhakikisha tunatengeneza utaratibu ambapo kila Halmashauri itatenga asilimia 30 ya manunuzi yake ya ndani kwa ajili ya vikundi vya akina mama na vijana.