Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 51 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 666 2023-06-20

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Primary Question

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA aliuliza: -

Je, ni lini Halmashauri ya Sikonge itapatiwa shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya kujenga Vituo vya Afya Ipole, Kipanga na Usunga?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Joseph George Kakunda, Mbunge wa Jimbo la Sikonge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali ilitenga shilingi milioni 500 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Tutuo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kuweka mipango Madhubuti ya ujenzi wa vituo vya afya vikiwemo vituo vya afya vya Ipole, Kapanga na Usunga ili kuendelea kutoa na kuboresha huduma za afya nchini.