Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 51 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 665 2023-06-20

Name

Dr. Florence George Samizi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Muhambwe

Primary Question

MHE.SYLIVIA F. SIGULA K.n.y. MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itapeleka fedha kumalizia ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Kizazi?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Florence George Samizi, Mbunge wa Jimbo la Muhambwe kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Katika mwaka wa fedha wa 2023/2024, Serikali imetenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Kizazi.