Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 32 Works, Transport and Communication Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi 423 2023-05-24

Name

Dr. David Mathayo David

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Same Magharibi

Primary Question

MHE. DKT. DAVID M. DAVID aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Mwembe – Mbaga hadi Mamba kwa kiwango cha lami?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. David Mathayo David, Mbunge wa Same Magharibi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuifanyia upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Mwembe – Mbaga hadi Mamba ambayo inaitwa Mwembe – Myamba – Ndungu yenye urefu wa kilometa 90.19. Baada ya usanifu kukamilika Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi.