Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 32 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 418 2023-05-24

Name

Dr. John Danielson Pallangyo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arumeru-Mashariki

Primary Question

MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO aliuliza: -

Je, ni lini mradi wa ujenzi wa soko la kisasa Tengeru utatekelezwa ili kuongezea mapato na kuboresha huduma kwa wananchi?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. John Danielson Pallangyo, Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Meru imetenga eneo la Madiira lenye ukubwa wa ekari
15.5 kwa ajili ya ujenzi wa soko litakalokuwa na miundombinu muhimu ya soko ikiwemo huduma za wafanyabiashara wadogo wadogo.

Mheshimiwa Spika, Halmashauri inaandaa michoro ya soko la Madiira na itakapokamilika itawasilisha Ofisi ya Rais – TAMISEMI kama mradi wa kimkakati kwa hatua zaidi.