Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 2 Works, Transport and Communication Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi 23 2023-04-05

Name

Dr. Florence George Samizi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Muhambwe

Primary Question

MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itajenga Daraja la Mto Lumpungu katika Jimbo la Muhambwe?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Florence George Samizi, Mbunge wa Muhambwe kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Mto Lumpungu unatenganisha nchi ya Burundi na Tanzania katika Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma kwenye Kijiji cha Kibuye, Kata ya Kumsenga. Kwa kuwa ujenzi wa daraja hili utahusisha nchi mbili Burundi na Tanzania, Serikali itaanzisha mazungumzo na nchi ya Burundi ili ziweze kukubaliana kuhusu ujenzi wa daraja hili, ahsante.