Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 23 Foreign Affairs and International Cooperation Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki 204 2022-05-16

Name

Ussi Salum Pondeza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chumbuni

Primary Question

MHE. ABDUL-HAFAR IDRISSA JUMA K.n.y. MHE. USSI SALUM PONDEZA aliuliza: -

Je, ni nchi ngapi zimeshafungua Ofisi zao za Ubalozi Jijini Dodoma baada ya zoezi la kuhamisha Makao Makuu ya Serikali Dodoma?

Name

Amb. Liberata Rutageruka Mulamula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Pondeza Mbunge wa Chumbuni, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, hadi sasa nchi tatu zimeshafungua Ofisi Ndogo za Ubalozi Jijini Dodoma. Nchi hizo ni Uingereza, Ujerumani na China. Hata hivyo, Wizara inaendelea kuzishawishi nchi nyingine kufungua Ofisi zao hapa Jijini Dodoma.

Mheshimiwa Spika, katika hatua nyingine baadhi ya Mashirika ya huduma za jamii na maendeleo ya Umoja wa Mataifa yameshafungua Ofisi zake Jijini Dodoma. Mashirika hayo ni pamoja na UNDP, UNICEF, UN Women, WFP, WHO, UNFPA, FAO, IFAD, IOM, UNAID, UNCDF na UNIDO.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha. (Makofi)