Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 16 Works, Transport and Communication Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 136 2022-05-05

Name

Nicholaus George Ngassa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Igunga

Primary Question

MHE. NICHOLAUS G. NGASSA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itafikisha mawasiliano ya simu katika Kata ya Kinungu, Isakamaliwa, Mtungulu, Kining’inila na Itumba?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Nicholaus George Ngassa, Mbunge wa Igunga, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) itafikisha huduma za mawasiliano ya simu katika Kata za Kinungu, Isakamaliwa, Mtungulu, Kining’inila na Itumba katika Jimbo la Igunga mwaka wa fedha 2022/2023 kupitia Mradi wa Tanzania ya Kidijitali.

Mheshimiwa Spika, Zabuni ya miradi hii itatangazwa kabla ya mwaka wa fedha wa 2021/2022 kukamilika. Ahsante.