Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 17 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 141 2022-05-06

Name

Sebastian Simon Kapufi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpanda Mjini

Primary Question

MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza watumishi katika Manispaa ya Mpanda hasa katika maeneo ya afya, elimu na maendeleo ya jamii?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Sebastian Simon Kapufi, Mbunge wa Mpanda Mjini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ina jumla ya watumishi 1,226 kati ya watumishi 1,773 wanaohitajika sawa na asilimia 69.1.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kuajiri watumishi kwa awamu ambapo katika mwaka wa fedha 2021/2022 watumishi 7,612 wa kada za afya na watumishi 9,800 wa kada za elimu wataajiriwa. Ahsante.