Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 10 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 82 2022-04-21

Name

Juliana Daniel Shonza

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka Watumishi wa Afya wa kutosha katika Kituo cha Afya cha Itaka?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwa niaba ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuajiri na kuwapeleka watumishi katika vituo vya kutolea huduma za afya kote nchini ambapo katika ajira za mwaka 2020/2021 Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi ilipelekewa watumishi 17 na kati yao watumishi Wawili walipelekwa Kituo cha Afya Itaka.

Mheshimiwa Spika, katika ajira za watumishi wa kada za afya 7,612 zilizotangazwa wiki hii, Kituo cha Afya Itaka kitapewa kipaumbele. Ahsante.