Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 10 Sitting 9 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 150 2023-02-10

Name

Zuena Athumani Bushiri

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itajenga skimu katika vijiji vya Maore, Mpirani, Kadando na Mheza?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo napenda kujibu swali la Mheshimiwa Zuena Athumani Bushiri, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali imepanga kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa skimu zilizopo katika vijiji vya Maore, Mpirani, Kadando na Mheza ili kupata gharama halisi za ujenzi. Baada ya zoezi la upembuzi yakinifu kukamilika, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji itatenga fedha katika bajeti ya mwaka 2024/2025 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji.