Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 10 Sitting 9 Community Development, Gender and Children Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 141 2023-02-10

Name

Tamima Haji Abass

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. TAMIMA HAJI ABASS aliuliza: -

Je, ni upi mkakati wa Serikali wa kutoa elimu kwa jamii dhidi ya udhalilishaji na ukatili wa watoto?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Tamima Haji Abass, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kupitia mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili kwa wanawake na Watoto, Serikali imeunda Kamati za Ulinzi wa Watoto na kuandaa vijarida na vitini vya kutoa elimu katika jamii kuhusu madhara ya ukatili, vyombo mbalimbali vya habari vinatoa vipindi vya kitaalamu kuhusu haki na ulinzi wa mtoto pia elimu ya athari za ukatili; walimu wa malezi na unasihi wamepata mafunzo ya kutoa elimu ya ulinzi wa watoto kwa walimu wenzao na wanafunzi; pia kupitia viongozi wa kijamii walio sehemu ya kamati ya jamii kwa kushirikiana na maafisa maendeleo, ustawi na elimu wanatumika katika kubadili mitazamo na fikra hasi za jamii, ahsante.