Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 10 Sitting 8 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 130 2023-02-09

Name

Noah Lemburis Saputi Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

MHE. NOAH L. S. MOLLEL aliuliza: -

Je, kuna mpango gani wa kutoa chakula cha bei nafuu kwa wananchi wa Jimbo la Arumeru Magharibi kutokana na athari za ukame?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Noah Lemburis Saputu, Mbunge wa Arumeru Magharibi kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) imeendelea kutoa chakula na kukiuza chini ya bei ya soko. Hadi kufikia tarehe 31 Januari, 2023 kiasi cha mahindi tani 24,975.152 zimepelekwa na kuuzwa katika Halmashauri 60 nchini katika vituo vya mauzo 116. Halmashauri ya Arumeru, kituo cha mauzo kimefunguliwa eneo la Kikatiti na jumla ya tani 6.28 zimeshauzwa kwa Wananchi.