Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 10 Sitting 7 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 111 2023-02-08

Name

Mwantumu Mzamili Zodo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MWANTUMU M. ZODO aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwawezesha Wakulima wa zao la Mwani ili kuongeza tija?

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mwantumu Zodo, Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2022/2023 Serikali imetenga fedha za program maalum ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) kupitia dirisha la Extended Credit Facility (ECF) kwa ajili ya kuwawezesha wakulima wa mwani pembejeo kwa mkopo wa masharti nafuu na usio na riba kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha kwa awamu ya kwanza, Wizara itatoa pembejeo za mwani zenye thamani ya shilingi 447,251,244 kwa wakulima 343 waliokwenye vikundi katika wilaya saba za Muheza, Pangani, Mtama, Mkuranga, Kilwa, Lindi Mjini na Mtwara Vijijini, ahsante.