Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 10 Sitting 6 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 93 2023-02-07

Name

Joseph Michael Mkundi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Primary Question

MHE. JOSEPH M. MKUNDI aliuliza: -

Je, ni lini Chuo cha VETA Ukerewe kitaanza kufanya kazi?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Michael Mkundi, Mbunge wa Jimbo la Ukerewe, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kukamilisha ujenzi wa Chuo cha VETA Ukerewe ili kiweze kutoa mafunzo yatakayowezesha vijana kujiajiri na kuajiriwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa chuo hiki upo katika hatua za mwisho za ukamilishaji ambapo ujenzi umefikia asilimia 97. Aidha, tayari Serikali imetoa fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa chuo hiki ili kianze kutoa mafunzo ya muda mfupi ifikapo mwezi Aprili, 2023.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru.