Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 10 Sitting 6 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 92 2023-02-07

Name

Emmanuel Peter Cherehani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ushetu

Primary Question

MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI aliuliza: -

Je, kuna mpango gani wa kujenga Chuo cha VETA Ushetu?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Emmanuel Peter Cherehani, Mbunge wa Jimbo la Ushetu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni azma ya Serikali kujenga Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) katika kila Mkoa na Wilaya nchini. Katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 100 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa vyuo vya VETA katika Wilaya 63 ambazo hazina vyuo hivyo. Kiasi hiki pia kitatumika katika ujenzi wa chuo cha VETA cha Mkoa wa Songwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Kahama ni miongoni mwa Wilaya zitakazojengewa Vyuo vya VETA ambapo kwa sasa Serikali ipo katika hatua za maandalizi ya ujenzi. Hivyo wananchi wa Jimbo la Ushetu watanufaika na Chuo cha VETA cha Wilaya ya Kahama.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.