Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 10 Sitting 6 Lands, Housing and Human Settlement Development Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 90 2023-02-07

Name

Justin Lazaro Nyamoga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Primary Question

MHE. NANCY H. NYALUSI K.n.y. MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itarudisha Shamba la Kijiji cha Ng’ang’ange kwa wananchi kufuatia mauziano kati ya EFATHA na Kijiji kutofuata sheria?

Name

Ridhiwani Jakaya Kikwete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chalinze

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Justin Nyamoga, Mbunge wa Kilolo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2003 Taasisi ya Efatha Ministry iliomba eneo lenye ukubwa wa ekari 200 katika Kijiji cha Ng'anga'nge kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi, Kilimo na Mifugo. Taratibu zote za utoaji eneo husika zilifuatwa ikiwemo Kikao cha Halmashauri ya Kijiji, Mkutano Mkuu wa Kijiji na Kamati ya kugawa ardhi ya Wilaya pamoja na fidia za mali zililipwa.