Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 10 Sitting 4 Lands, Housing and Human Settlement Development Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 62 2023-02-03

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza: -

Je, Serikali ina kauli gani juu ya maeneo ya ardhi yanayotumika na Serikali au Taasisi zaidi ya miaka 12 yakiwa hayana hatimiliki?

Name

Ridhiwani Jakaya Kikwete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chalinze

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, naomba kujibu swali Na. 62 lililoulizwa na Mheshimiwa Boniphace Mwita Getere, Mbunge wa Bunda, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kuwa maeneo mengi yanayomilikiwa na Taasisi za Umma yana hatimiliki. Hata hivyo, Serikali kwa nyakati tofauti imekuwa ikitoa maelekezo kwa Taasisi na Idara za Umma kuhakikisha maeneo yao yanapangwa, kupimwa na kupatiwa hatimiliki.