Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 10 Sitting 4 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 51 2023-02-03

Name

Josephine Johnson Genzabuke

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itatoa vibali ili kuajiri walimu na kuondoa upungufu wa walimu uliopo nchini?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Josephine Johnson Genzabuke, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kutatua na kukabiliana na changamoto ya upungufu wa walimu nchini kwa kutoa vibali vya ajira za walimu ambapo kwa mwaka wa fedha 2020/2021 iliajiri walimu 14,949 na mwaka wa fedha 2021/2022 iliajiri walimu 9,800.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea na mpango wa kuajiri watumishi wakiwemo walimu ili kukabiliana na upungufu kulingana na mahitaji na upatikanaji wa fedha.