Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 10 Sitting 3 Lands, Housing and Human Settlement Development Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 45 2023-02-02

Name

Tarimba Gulam Abbas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kinondoni

Primary Question

MHE. TARIMBA G. ABBAS aliuliza: -

Je, nini kauli ya Serikali kuhusu majengo yaliyopo maeneo ya Mkoa wa Dar es Salaam ambayo ujenzi wake umesimama kwa muda mrefu?

Name

Ridhiwani Jakaya Kikwete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chalinze

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, naomba kujibu swali namba 45 lililoulizwa na Mheshimiwa Tarimba Abbas Mbunge wa Kinondoni kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, maelekezo ya Serikali ni kwamba majengo yote yaliyosimama yaendelezwe kwa kikamilifu kama ilivyoainishwa kwenye milki zao na vibali vya ujenzi ili majengo hayo yasitumike kwa matumizi yasiyofaa.