Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 10 Sitting 1 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 10 2023-01-31

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kudhibiti madalali wanaodalalia mazao ya wananchi yakiwa shambani kwa bei wanazozitaka?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Saashisha Elinikyo Mafuwe Mbunge wa Jimbo la Hai kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza mpango wa uanzishwaji wa vituo rasmi vya uuzaji na ununuzi wa mazao ya kilimo karibu na maeneo ya uzalishaji ili kumuwezesha mkulima kuuza mazao yake kwa bei ya soko na kuzuia uuzwaji wa mazao shambani. Vilevile Serikali inaendelea na mpango wa ujenzi wa ghala za kuhifadhia mazao katika maeneo ya uzalishaji ili kuwezesha wakulima kuhifadhi na kuuza mazao yao.