Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 10 Sitting 1 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu 1 2023-01-31

Name

Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. THEA M. NTARA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itatangaza kima cha chini cha mishahara kwa Wafanyakazi wa Serikali na mashirika binafsi?

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCAL P. KATAMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Thea Medard Ntara, Mbunge wa Viti Maalum kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ninapenda kulijulisha Bunge lako tukufu kuwa kima cha chini cha mshahara kwa sekta ya umma kilitangazwa tarehe 13/5/2022 na utekelezaji wake ulianza tarehe 1 Julai, 2022. Kwa upande wa sekta binafsi kima cha chini cha mshahara kilitangazwa tarehe 25/11/2022 kwenye Gazeti la Serikali Na. 687 baada ya Bodi ya Kima cha Chini cha Mishahara kukamilisha utafiti na kutoa mapendekezo ya viwango kwa Sekta Binafsi ambayo yaliridhiwa na Baraza la Ushauri kuhusu Kazi, Uchumi na Jamii (LESCO). Utekelezaji wake unaanza rasmi Tarehe 1 Julai, 2023.