Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 7 Community Development, Gender and Children Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 59 2022-04-14

Name

Husna Juma Sekiboko

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZAINAB A. KATIMBA K.n.y. MHE. HUSNA J. SEKIBOKO aliuliza: -

Je, kuna athari gani za kijamii kwa watumishi wenza kuishi mbali na watoto wao?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Husna Juma Sekiboko, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, familia ni taasisi muhimu sana katika kuleta ustawi kwa jamii na Taifa kwa ujumla. Ni kweli kuwa yapo madhara ya kijamii kwa watumishi wenza kuishi mbali na watoto wao madhara hayo ni kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kuongezeka kwa vitendo vya ukatili kwa watoto majumbani; kukosa malezi chanya inayopelekea watoto kuathirika kisaikolojia; watoto kutokupata lishe bora inayopelekea udumavu na mmomonyoko wa maadili na kuvunjika kwa ndoa kunakosababisha watoto wa mtaani. Ahsante.