Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 9 Sitting 8 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 121 2022-11-09

Name

Oran Manase Njeza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbeya Vijijini

Primary Question

MHE. ORAN M. NJEZA aliuliza: -

Je ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Ndaki ya Sayansi ya Afya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Mamlaka ya Mji wa Mbalizi?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali na Mheshimiwa Oran Manase Njeza, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimeanza hatua za awali kwa kuwasilisha kwa Msajili wa Hazina maombi ya kupewa ardhi yenye ukubwa wa hekari 2000 kwenye eneo lililokuwa shamba la Tanganyika Packers kwa ajili ya ujenzi. Kwa sasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinaendelea kufuatilia maombi haya kwa Msajili wa Hazina.

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa Ndaki ya Sayansi ya Afya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam - Mbalizi utaanza mara moja pale upatikanaji wa ardhi utakapokamilika.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.