Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 9 Sitting 7 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 96 2022-11-08

Name

Dr. Paulina Daniel Nahato

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. PAULINA D. NAHATO aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itawalipa Wahadhiri wote nchini malimbikizo yao ya miaka ya nyuma?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Paulina Daniel Nahato, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali hulipa malimbikizo ya watumishi wote wa Serikali wakiwemo Wahadhiri baada ya kujaza fomu za malimbikizo (arrears clearance forms). Mara baada ya mtumishi kukamilisha kujaza fomu hizo na kuwasilishwa, madai yao hupelekwa Ofisi ya Rais, Management ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na baadaye Hazina kwa ajili ya malipo.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Septemba, 2022, Serikali imelipa jumla ya Sh.1,172,429,710 kwa ajili ya malimbikizo ya Wahadhiri. Serikali itaendelea kulipa malimbikizo ya Wahadhiri kulingana na bajeti ya fedha kwa mwezi na mwaka husika.