Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 9 Sitting 7 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 94 2022-11-08

Name

Nicholaus George Ngassa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Igunga

Primary Question

MHE. NICHOLAUS G. NGASSA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itajenga Skimu ya Umwagiliaji ya Igurubi katika Jimbo la Igunga?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Nicholaus George Ngassa Mbunge wa Igunga, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali kupitia Tume ya Taifa ya umwagiliaji imepanga kufanya mapitio, upembuzi yakinifu na usanifu kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa ujenzi wa Bwawa la Umwagiliaji katka Skimu ya Igurubi. Aidha, mara baada ya kukamilika kwa upembuzi yakinifu na usanifu na gharama ya ujenzi kujulikana, Tume ya Taifa ya Umwagiliaji itatenga fedha katika bajeti ya mwaka 2024/2025 kwa ajili ya ujenzi wa bwawa hilo.