Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 9 Sitting 7 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 92 2022-11-08

Name

Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vwawa

Primary Question

MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itaanza kujenga soko la mazao la Kimataifa katika eneo la Mbimba TACRI Vwawa ili Wananchi wapate soko la uhakika?

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa kilimo na ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Japhet Ngailonga Hasunga, Mbunge wa Vwawa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi imetenga ekari 25 kwa ajili ya ujenzi wa soko ambapo eneo hilo limeshafanyiwa upembuzi yakinifu kwa kushirikiana na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). Aidha, gharama za ujenzi wa soko hilo ni takribani shilingi 14,117,640,924.91. Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.