Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 4 Works, Transport and Communication Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi 38 2022-04-11

Name

Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza: -

Je, ni nani mwenye jukumu la kusafisha mifereji na kuzibua makaravati ya barabara zinazojengwa chini ya TARURA au TANROADS?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Naghejwa Livingstone Kaboyoka, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, jukumu la usafi wa barabara na mifereji ikiwa ni pamoja na kuzibua makaravati ni la msimamizi wa barabara husika. Hivyo, kwa barabara za TANROADS mhusika ni TANROADS na za TARURA mhusika ni TARURA.