Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 4 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 31 2022-04-11

Name

Mwantumu Mzamili Zodo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MWANTUMU M. ZODO aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itafanya ukarabati wa Hopsitali ya Wilaya ya Pangani?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshemiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mwantumu Mzamilu Zodo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imetenga shilingi bilioni 21 kwa ajili ya kufanya ukarabati wa Hospitali kongwe 21 ikiwemo Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani. Aidha, kupitia mpango huo, kila hospitali kongwe imetengewa shilingi bilioni moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kukarabati hospitali za Halmashauri ambazo miundombinu yake imechakaa ili kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini kote.