Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 3 Community Development, Gender and Children Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 24 2022-04-08

Name

Nusrat Shaaban Hanje

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NUSRAT S. HANJE aliuliza: -

Je? Serikali ina mkakati gani wa kuzuia ukatali wa kijinsia na utumikishwaji wa watoto katika makambi yanayotarajiwa kujengwa ili kuwezesha ujenzi wa Bomba la Mafuta Hoima Tanga?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Spika, ahsante. Napenda kujibu swali la Mheshimiwa Nusrat Shaaban Hanje, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha vitendo vya ukatili wa kijinsia na utumikishaji wa watoto vinakomeshwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo mradi wa bomba la mafuta Hoima Tanga, kupitia MTAKUWWA Wizara yangu imejipanga kuimarisha na kuzijengea uwezo Kamati za Ulinzi na Usalama kwa watoto kwa vile Serikali itaendelea kutumia vyombo vya dola kuhakikisha wale wote wanaotumikisha watoto na kufanya vitendo vya ukatili wanachukuliwa hatua za kisheria. (Makofi)