Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 9 Sitting 6 Works, Transport and Communication Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 81 2022-11-07

Name

Kenneth Ernest Nollo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bahi

Primary Question

MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itaanza programu ya kuunda na kurusha setilaiti?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kenneth Ernest Nollo, Mbunge wa Bahi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa nchi kuwa na Setilaiti, hivyo, mwaka huu wa fedha Serikali imeanza utaratibu wa awali utakaowezesha kuunda na kurusha setilaiti angani. Ili kuwezesha kufikia azma hiyo, Serikali tayari imeandaa andiko dhana na kuunda timu ya wataalam watakaoshauri aina ya setilaiti tutakayorusha angani itakayoendana na mahitaji halisi ya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, ni matarajio kuwa timu hiyo itakamilisha kazi ya uchambuzi kisha kuwasilisha mapendekezo yake Serikalini kwa hatua za kimaamuzi ndani ya mwaka huu wa fedha. Ahsante.