Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 9 Sitting 4 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 54 2022-11-04

Name

Ally Mohamed Kassinge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kusini

Primary Question

MHE. ALLY M. KASSINGE aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itaanza mchakato wa ujenzi wa Bandari ya Uvuvi katika Mji wa Kilwa Masoko?

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ally Mohamed Kassinge Mbunge wa Kilwa Kusini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imeshaanza ujenzi wa Bandari ya Uvuvi katika eneo la Kilwa Masoko Mkoani Lindi. Mkataba wa ujenzi wa Bandari hiyo ulisainiwa tarehe 07 Juni, 2022 kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Mkandarasi ambaye ni Kampuni ya M/S China Harbour Engineering. Aidha, maandalizi ya awali ya ujenzi wa Bandari hiyo yameanza na ujenzi unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 24. Ahsante.