Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 9 Sitting 4 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 50 2022-11-04

Name

Simon Songe Lusengekile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busega

Primary Question

MHE. SIMON S. LUSENGEKILE aliuliza: -

Je, ni lini Barabara ya kutoka Igalukilo - Sayaka inayounganisha Mikoa ya Mwanza na Simiyu itahamishiwa TANROADS?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Simon Songe Lusengekile, Mbunge wa Jimbo la Busega, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Sheria ya Barabara, Namba 13 ya mwaka 2007 na Kanuni zake za mwaka 2009, imeainisha vigezo na utaratibu wa kuhamisha barabara ili iwe chini ya TANROADS ambapo barabara inaweza kupandishwa au kuteremshwa toka daraja moja kwenda daraja lingine.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais, TAMISEMI inaielekeza Halmashauri ya Wilaya Busega kupitia TARURA kufuata utaratibu huo ili kuiweka barabara hiyo katika mpango wa kupandishwa hadhi na kuwa ya mkoa.